MARUFUKU KUANDAMANA DISEMBA 09- JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yanayohamasishwa katika mitandao ya kijamii kwa kuyaita maandamano ya amani ya Disemba 09, 2025 kutokana na kutofuata taratibu kulingana na sheria ya Polisi pamoja na kujaa viashiria vingi vya uhalifu na uvunjifu wa sheria na taratibu. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Disemba 05, 2025 kwa Vyombo vya habari na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, imesema hatua hiyo imefikiwa pia kutokana na mbinu za kihalifu ambazo zimebainika wakihamasishana kuzitumia kuanzia tarehe 09 Disemba, maandamano hayo yamekosa aifa za kisheria kuyaruhusu kuweza kufanyika. "Mtu yeyote anayepanga kufanya maandamano sheria inamtaka kuwasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa maandamano hayo kwa Afisa Polisi msimamizi wa eneo husika akiainisha sehemu yatakayofanyika maandamano hayo, muda, madhumuni na maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi mara kwa mara kwenye gazeti la serikali." Imesema taarifa ya Polisi. Polisi pi...